Aliyekuwa Waziri wa Fedha Henry Rotich ateuliwa mshauri wa Rais

Rais William Ruto amemteua aliyekuwa Waziri wa Fedha Henry Rotich kuwa mshauri mkuu wa masuala ya pesa za umma na bajeti katika afisi yake.

Rotich alihudumu kama Waziri wa Fedha katika serikali ya Rais Uhuru Kenyatta kuanzia mwaka 2013.

Mwezi Julai, 2019, Rotich na katibu katika Wizara ya Fedha wakati huo Dkt. Kamau Thuge walisimamishwa kazi kwa tuhuma za ufisadi.

Aliondolewa kwenye wadhifa huo Januari 14, 2020 na mahali pake kuchukuliwa na Ukur Yatani.

Mwezi Disemba mwaka 2023, mahakama ya Milimani ilimwondolea lawama Rotich na wenzake 8 kwenye kesi ya ufisadi ya shilingi bilioni 63 za miradi ya mabwawa ya Aror na Kimwarer.

Hakimu Eunice Nyutu aliondolea washukiwa hao lawama kwa kile alichokitaja kuwa upande wa mashtaka kushindwa kutoa ushahidi wa kutosha.

Leave a Reply